Bashite achafua hewa CCM, amrushia kijembe JK, asema "sio utaratibu kwa wastaafu kila siku kuongeaongea", amwamuru Waziri Mkuu Majaliwa kumaliza kero za ardhi ndani ya miezi 6
Kama hotuba ya Bashite wiki iliyopita ambayo ilikuwa ya kwanza tangu ateuliwa na Mama Samia kuwa mwenezi wa CCM iliwaacha baadhi ya watu wakiwa na matumaini kwamba “labda amepitiwa tu, lakini kuwekwa benchi kumembadili”, hotuba yake ya pili hapo jana bila shaka itakuwa imeondoa kabisa hisia hizo.
Kabla ya kuingia ndani zaidi, soma uchambuzi huu wa kiintelijensia kuhusu hotuba hiyo ya kwanza ya Bashite wiki iliyopita
Katika hotuba yake ya jana sio tu alithibitisha kuwa hajabadilika bali pia alionyesha bayana kuwa kuna uwezekano akawa mtu hatari zaidi ya alivyokuwa enzi za JPM, kitu ambacho Jasusi alikibashiri kwenye uchambuzi wa awali kuhusu kuteuliwa kwake.
Makala hii inachambua kwa kifupi baadhi ya kauli za Bashite alizotoa jana huko Dodoma ambako alipokelewa rasmi baada ya mapokezi ya wiki iliyopita jijini Dar.