Dear ACT-Wazalendo (@ACTWazalendo), adui yenu katika hoja ya "uhuru wa Zanzibar" si Watanganyika bali CCM mnayoshirikiana nayo huko Visiwani.
ACT-Wazalendo ni moja ya vyama vichache kabisa vya upinzani si barani Afrika tu bali pengine duniani kwa ujumla vilivyoweza kupata mafanikio makubwa katika muda mfupi sambamba na kustahimili misukosuko mbalimbali inayoziandama siasa za upinzani. Kimsingi, chama hicho ndio chama kikuu cha upinzani Tanzania kwa mujibu wa idadi ya wabunge kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kwa Watanzania wengi, ACT-Wazalendo sio tu kinaweza kuwa mbadala wa Chadema kuing’oa CCM madarakani bali pia ACT-Wazalendo inaweza kuwa mbadala wa CCM pia. Na japo kijiografia Zanzibar ni ndogo mara kadhaa ukulinganisha na “Tanzania Bara”, ACT-Wazalendo imefenikiwa kwa kiasi kikubwa huko Zanzibar kuthibitisha kuwa inaweza kuwa chama tawala badala ya CCM.
Kukua na hatimaye kuimarika kwa chama hicho huko Zanzibar kulichangiwa na uamuzi wa mwanasiasa maarufu, Marehemu Seif Sharif Hamad a.k.a Maalim Seif kujiunga na ACT-Wazalendo baada ya kufukuzwa na kilichokuwa chama kikuu cha upinzani visiwani humo cha CUF ambacho Maalim Seif alishiriki kukiasisi.
Sasa unaweza kuwa paid subscriber wa vijarida vya Barua ya Chahali, Ujasusi Blog na AdelPhil Online Academy kwa gharama nafuu zaidi. Cha kufanya, subscribe kwenye akaunti ya Jasusi huko Instagram, kisha mpatie email yako au namba ya Whatsapp, utachagua kutumiwa kijarida kwa email au kwa Whatsapp
Akiwa mwanasiasa mwenye nguvu kubwa kuliko wote Zanzibar, Maalim Seif aliandika historia ya kuiwezesha ACT-Wazalendo kuwa “chama kikubwa kama CUF” kwa muda mfupi kabisa, Waingereza wanasema “overnight.” Na kuimarika kwa chama hicho kulipelekea kudhoofika kwa CUF, chama ambacho kwa sasa kimebaki jina tu kama vilivyo vyama vingine vingi vya upinzani nchini Tanzania, kama vile NCCR-Mageuzi, TLP, nk.