Dear Chadema na ACT-Wazalendo, mlipoamua kushiriki "uchafuzi" huu mlikuwa mnategemea miujiza?
Ikiwapendeza, fanyeni "political outreach" nje ya vyama vyenu mpate maoni kuhusu mbinu mbadala kuhusu kuikabili CCM kwani mnazotumia sasa zimefeli
Tangu mchakato wa uchaguzi wa serikali za vijiji, mitaa na vitongoji uanze, kitu kimoja ambacho kinatawala mno ni malalamiko mfululizo ya vyama vikuu vya upinzani vya Chadema na ACT-Wazalendo kuhusu rafu zinazofanywa na CCM kupitia TAMISEMI.
Ni muhimu kupigia mstari kwamba, kwanza, ni haki ya kikatiba ya vyama hivyo kulalamikia kasoro wanazoziona kwenye …