Guest Column: Dear Mama Samia, Ujumbe Kutoka Kwa Kada wa Chama Chenu: "CCM Tujisahihishe au Watanzania Watatusahihisha."
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Miaka 22 imepita sasa tangu Baba wa Taifa atutoke, Tanzania imeendelea kuwepo na hakika itaendelea kuwepo sana. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa rais wa kwanza wa Taifa letu aliacha hazina ya maongozi na mawazo chanya yenye kusaidia kulibeba Taifa letu katika nyakati zote hata zile ngumu z…