Barua Ya Chahali
Jasusi
Heri Ya Mwezi Mpya Wa Machi: Fahamu Mbinu Hii Kila Uanzapo Wakati (Saa/Siku/Wiki/Mwezi/Mwaka) Mpya
0:00
Current time: 0:00 / Total time: -5:00
-5:00

Heri Ya Mwezi Mpya Wa Machi: Fahamu Mbinu Hii Kila Uanzapo Wakati (Saa/Siku/Wiki/Mwezi/Mwaka) Mpya

Mbinu husika inahusiana na falsafa ya Stoicism, ambayo nayo nitaitafutia muda maalum wa kuieleza kwa upana. Na katika Stoicism kuna kitu kinachofahamika kama "Premeditatio Malorum," kwa kimombo "the premeditation of the evils and troubles that might lie ahead." Kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili ni ile hali ya kuwa na utambuzi wa mambo mabaya yanayoweza kutokea huko mbeleni.