Huduma ya intaneti ya kasi ya 'Starlink' ya Elon Musk: Waziri @Nnauye_Nape aeleza kuwa serikali ipo tayari ila kinachosubiriwa ni bilionea huyo kuwasilisha nyaraka husika
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa ufafanuzi kuhusu kuchelewa huduma ya kasi ya intaneti ya Satarlink inayomilikiwa na mfanyabiashara tajiri duniani Elon Musk kuchelewa kuwasili nchini Tanzania.
Awali mfanyabiashara mmoja wa nchini Afrika Kusini, Mike Coudrey alimwiti Elon kumshauri ahakikishe huduma ya S…