Huku kukiwa hakuna dalili za Rais Samia kutekeleza matakwa ya Chadema kufikia Septemba 21, sababu mbili muhimu zinazoweza kuwafanya polisi wasizuwie maandamano Septemba 23
Zikiwa zimesalia siku 5 kabla ya kutimia Septemba 21, tarehe ambayo Chadema waliitangaza kama deadline ya kuhakikisha Rais Samia Suluhu anatimiza matakwa yao kadhaa, hakuna dalili zozote kuwa mkuu huyo wa nchi ana mpango wowote wa kufanya hivyo.
Kujikumbusha kuhusu matakwa ya Chadema, rejea makala hii
Kadhalika, makala hii chini inaeleza kwa upana zaidi kwanini ni vigumu kwa Rais Samia kutimiza matakwa hayo ya Chadema
TANGAZO
Katika mazingira ya kawaida, uamuzi wa Rais Samia kukataa matakwa unamaanisha kuwa Chadema wataendelea na mpango wao wa kuandamana ifikapo Septemba 23.
Hata hivyo, tayari jeshi la polisi limetangaza kuwa maandamano hayo ni haramu.
Lakini kijarida hiki kinakuhabarisha kuhusu masuala mawili muhimu yanayoweza kupelekea polisi wasizuwie maandamano hayo endapo yatafanyika.