Jinsi "pattern of life intelligence" ilivyowawezesha CIA kumuua bosi wa Al-Qaeda Ayman al-Zawahiri, na angalizo kwa "tunaoendelea kuwindwa na watesi wetu"
Moja ya maswali nayoulizwa mara kwa mara ni pamoja na hili, “jasusi, Mwendazake ameshaondoka, na watu wake wengi wameondolewa. Na sasa nchi ipo chini ya Mama Samia, je bado maisha yako yapo hatarini? Unaweza kurudi Tanzania?”
Kabla ya kujibu swali hilo, nielezee kuhusu jinsi kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri, alivyouawa huko Afghanistan mwishoni mwa wiki iliyopita.
Japo mie si gaidi, kwa miaka kadhaa nimekuwa mtu ninayewindwa. Na huko nyuma yameshafanyika majaribio kadhaa ya kunitoa uhai.
Kwahiyo, kwa kiasi flani kuna mfanano wa jinsi Zawahiri alivyokuwa akiishi - alikuwa anawindwa na Marekani tangu mwaka 1998 alipoongoza mashambulizi ya kigaidi kwenye balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi, ambapo zaidi ya watu 200 waliuawa.