#JinsiYaKuwaMtuBora: Vitu Vinane Ambavyo Hujachelewa Kujifunza Maishani
Ufafanuzi kidogo. Kwenye masuala ya ujasusi, mie ni jasusi wako. Kwenye utumishi, mie ni mtumishi wako. Lakini kwenye haya masuala ya Jinsi ya Kuwa Mtu Bora aka “personal development” kwa kimombo, mie ni kocha wako. Kwanini “kocha”? Kwa sababu kuna fani inaitwa “ukocha wa maisha”, kwa kimombo “life coach.” Na hicho ndicho hasa nachofanya katika hizi koz…