Katiba Mpya Itapatikana, Tume Huru ya Uchaguzi Pia Itapatikana Lakini Si Kwa Matusi Bali Majadiliano
Jana nilifanya maongezi marefu na kada mmoja wa Chadema, daktari kitaaluma. Huyu msomi alinilaumu juzi baada ya mie kuwakemea wanaofanya siasa za chuki. Yeye alitaka niwakemee kwanza “waliosababisha hao wenye chuki wawe na chuki.”
Nikajitahidi kumuelimisha kwamba “two wrongs don’t make a right,” yaani “kwa vile kuna kosa lilishafanyika kabla, haimaanish…