Kenya: Watanzania wengine watano wakamatwa Garissa wakielekea Somalia kujiunga na al-Shabaab
Raia watano wa Tanzania waliotambuliwa kwa majina ya Muhamed Jahad Farah, Nadrik Mbwana Salumi, Saad Suleiman Saleh, Ali Issa Ali na na raia wa Uganda Hassan Tourabih Kintosa walikamatwa mjini Garissa, nchini Kenya, wakielekea Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab.