Kifahamu kikosi cha Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania kinachohusika na ulinzi wa viongozi (PSU) - sehemu ya pili: takriban kila mtu anatamani kuwa bodigadi wa kiongozi, je unajiungaje?
Karibu katika sehemu hii ya pili na ya mwisho ya makala kuhusu kikosi cha Idara ya Usalama wa taifa kinachohusika na ulinzi wa viongozi. Kikosi hicho kinafahamika kama PSU ikiwa ni kifupi cha Presidential Security Unit, yaani kikosi cha ulinzi wa Rais.
Kwa minajili ya kuelewa vizuri makala hii, inashauriwa usome kwanza sehemu ya kwanza
Kama ilivyoahidiwa kwenye hitimisho la sehemu ya kwanza ya makala hii, sehemu hii ya pili inaangalia pamoja na mambo mengine jinsi gani hasa maafisa usalama wa taifa walio mafunzoni wanavyochujwa na kuingia kwenye kikosi hicho cha ulinzi.
Kadhalika, makala inajibu swali linaloulizwa mara kwa mara kuhusu uwezekano wa kujiunga na PSU au Idara ya Usalama wa Taifa kwa ujumla.