Kifo cha Prigozhin: mkutano kati yake na Putin unaosemekana kuwa ndio "ulipitisha hukumu ya kifo" cha bosi huyo wa jeshi la mamluki la Wagner
Mnamo Agosti 23, miezi miwili baada ya uasi wake mfupi, Yevgeny Prigozhin aliuawa katika ajali ya ndege.
Sababu haijulikani, lakini Rais wa Urusi Vladimir Putin anashukiwa kupanga ajali hiyo.
Ikiwa ndivyo, mchakato wa kumwondoa Prigozhin unaweza kuwa umeanza katika mkutano wa Kremlin siku baada ya ghasia zake.