Kinyang'anyiro cha urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania urais wa Muungano?
Kwa kiasi kikubwa, siasa za Tanzania zimejikita zaidi kwenye chaguzi, hususan uchaguzi mkuu. Kwamba vyama vya siasa hutumia muda mwingi kujiandaa na chaguzi kiasi kwamba kuna dhana kwamba haviwatumikii wananchi vya kutosha kutokana na hilo.
Lakini lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Na katika nchi za kidemokrasia, kushika dola kunaweze…