Kozi ya Open Source Intelligence #OSINT kwa lugha ya Kiswahili: kusaka taarifa kwa kuidukua Google (Google hacking)
Masomo yaliyopita yalihusu anwani feki za baruapepe; sura (DP) feki; burner phone; vivinjari (browsers) vya upelelezi wa OSINT.
Katika kuhitimisha somo la 9 lililohusu injini tafuti (search engines) vivinjari (browsers), ilielezwa kuwa litaendelea katika somo lijalo. Kwahiyo somo hili litamalizia tulipoishia kabla ya kutambulisha moja ya nyenzo muhimu kabisa kwenye upelelezi wa OSINT yaani “kuidukua Google” (Google hacking).