Kutekwa, kuteswa, kuuawa kwa Mzee Ali Kibao: huku ukimya wa Lissu ukiibua maswali, baadhi wakerwa na "upole" wa Mbowe kwa Masauni
Makala hii ina sehemu mbili. Ya kwanza inazungumzia ukimya wa Mheshimiwa Tundu Lissu kufuatia kutekwa, kuteswa na hatimaye kuuawa kwa kiongozi mwandamizi wa Chadema, Mzee Ali Mohamed Kibao.
Sehemu ya pili inahusu “upole” wa Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa Waziri Masauni hapo jana katika msiba wa Marehemu Kibao.
TANGAZO
Wakati bado haijaingia akilini kwamba kiongozi mwandamizi wa Chadema, marehemu Ali Mohamed Kibao, angeweza sio tu kutekwa, kuteswa na kuuawa bali pia maiti yake kumwagiwa tindikali, kumeibuka sintofahamu kutokana na ukimya wa Makamu Mheshimiwa Tundu Lissu.