Kwa mara ya kwanza ktk historia TZ, Jaji amtuhumu Rais kuvunja Katiba: uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu tuhuma za Jaji Stella Mugasha vs Rais Samia kumuongezea mkataba Jaji Mkuu aliyepaswa kustaafu
Jana ilisambaa barua iliyoelezwa kuandikwa na Jaji Stella Mugasha wa Mahakama ya Rufani ikitamka bayana kuwa Rais Samia Suluhu amevunja katiba kwa kumuongezea muda Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ambaye alipaswa kustaafu baada ya kutimiza muda wa ksuataafu tarehe 15/06/2023.
Soma barua husika kisha pata uchambuzi wa kiintelijensia wa tukio hili la kihistoria
Tathmini ya kiintelijensia
Ikumbukwe tu kuwa sio tu kwamba tuhuma hizo za Jaji Mugasha ni za kwanza kabisa katika historia ya Tanzania kwa jaji kumtuhumu Rais kuvunja katiba, bali pia zimetokea wakati Rais Samia akilalamikiwa kuhusu mkataba kati ya Tanzania na Dubai ambao baadhi ya watu wanadai kuwa "nchi imeuzwa”.