Lugha gongana sakata la mkataba wa bandari: wakati Waziri Mbarawa akidai kuwa mkataba utazalisha ajira zaidi ya elfu 70, "wazee wa minyama" waliopo Dubai wasema DP World ni mwendo wa mashine tu 🤔
Wanasema “ukiona manyoya ujue kaliwa”. Ni msemo unaoweza kuendana na muktadha wa suala la mkataba wa uendeshaji wa bandari kati ya serikali ya Tanzania na Dubai, ambapo jana kuliibuka lugha gongana iliyozua mjadala mrefu.
Awali, Waziri Makame Mbarawa alidai kuwa mkataba huo utazalisha ajira zaidi ya elfu 71.