Mbinu za kijasusi unazoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku: mbinu ya pili - jinsi ya kuwa "MTU WA MACHALE" (Hisia ya Sita)
Huu ni mwendelezo wa mfululizo wa makala zitakazokufahamisha mbinu mbalimbali za kijasusi/kishushushu/kiintelijensia unazoweza kuzitumia katika maisha yako ya kila siku.
Makala hii ni ya pili katika mfululizo huu. Endapo hukubahatika kusoma makala iliyopita ambayo ilikuwa na mbinu maalum kwa “vijana singo, wenye aibu” soma hapa
Katika makala hii, utafundishwa mbinu moja muhimu sana katika maisha ya Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa aka shushushu aka jasusi. Kuanzia hapa hadi kufikia mwisho wa makala hii, neno litakalotumika ni jasusi pekee. Na mbinu husika ni MACHALE, au kwa neno rahisi ni “hisia ya sita”.
Urahisi wa mbinu hii ni kwamba haihitaji nguvu nyingi kui-develop hadi kiwango ambapo hata wewe ambaye hujapitia kozi yoyote ya ujasusi, ukamudu kuwa na machale kama jasusi halisi.
Lakini kabla ya kuingia kwenye mbinu husika, machale au hisia ya sita ni nini hasa? Kwa mtaani, mtu mwenye machale ni yule ambaye ni kama anafahamu kuhusu tukio (mara nyingi hasi) kabla halijatokea. Utasikia wanasema “dah jama ana machale sana” wakimaanisha kuwa ana uwezo wa kufahamu - na mara nyingi kuepuka - jambo/tukio lisilofaa kabla halijatokea.
Ofkoz, machale pia hutumika hata kwenye vitu ambavyo kwa ujumla ni hasi, kwa mfano jinsi wazinzi wanavyotumia machale kukwepa kufumaniwa. Kama ilivyoelezwa kwenye makala iliyopita, mbinu hizi zinaweza kutumiwa kwa nia nzuri au mbaya. Na ni juu ya mtu kutambua athari za kutumia mbinu hizi kwa nia mbaya.
Hisia 5 za binadamu
Binadamu “wa kawaida” ana hisia tano.
Ya kwanza ni harufu ambayo hutumia nyenzo ya pua kubaini.
Hisia ya pili ni ladha ambayo hutumia nyenzo ya ulimi na/au mdomo
Hisia ya tatu ni mwanga ambayo hutumia macho
Hisia ya nne ni sauti ambayo hutumia nyenzo ya masikio
Na hisia ya tano ni kugusa/kuguswa (touch) ambayo hutumia zaidi nyenzo ya ngozi
Kwa kifupi, machale au hisia ya sita ni kitu cha zaidi ya hivyo vitano, ambapo unaweza kunusa bila kutumia pua, kuona bila kutumia macho, kugusa/kuguswa pasi ngozi kuhusika, kusikia bila kutumia masikio na kulamba pasi kutumia ulimi.
Lakini kama ilivyoelezwa mwanzo, hisia ya sita humwezesha mwenye nayo kutambua yajayo kabla hayajatokea bila kuwa na taarifa yoyote ile.
Kama katika familia yenu kuna mapacha waliofanana kila kitu (identical twins), unaweza kubaini kuwa japo Kulwa yupo mbali na Doto, na hawana mawasiliano yoyote, wawili hao wanaweza kufanya tendo kwa wakati mmoja kana kwamba waliambiana kabla.
Lakini hata bila ya kuwa mapacha, mara nyingi kama kuna tukio kubwa maishani hususan misiba, watu wengi huota ndoto zenye mikusanyiko ya watu au wengine huota ndoto za kupita makaburini.
Kadhalika, mara nyingi tu unaweza kumfikiria mtu flani, na ghafla mtu huyo akakupigia simu au akatokea kana kwamba ulimuita.
Mifano ya hisia ya sita au machale ni mingi na haiwezi kutosha kwenye makala moja kama hii. Na lengo si kuiorodhesha bali kukupatia mbinu za kui-develop