Mbunge huyu ni jasusi wa nchi moja jirani, ambaye Idara ya Usalama wa Taifa inafahamu kuwa ni pandikizi, anajaribu kujiweka karibu na Mama Samia
Kuna mambo yanatia hasira sana kuhusu nchi yetu. Ni mengi, lakini kwa Jasusi, jambo ambalo sio tu linamtia hasira bali pia linamtatiza sana ni kutapakaa kwa watendaji mbalimbali wa serikali ambao wanatumikia Idara za Usalama wa Taifa za nchi nyingine.
Mwezi uliopita, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda alimfahamisha Rais Samia Suluhu HADHARANI kuhusu janga hilo.
Nimeandika HADHARANI kwa herufi kubwa kwa sababu Mkuu wa Majeshi ni mjumbe wa Kamati ya Usalama wa Taifa, na angeweza kuliongelea huko FARAGHANI, lakini akaliweka hadharani, ikimaanisha kuwa kuna walakini kwa mamlaka zinazopaswa kushughulikia tatizo hilo.
Na kwa hakika wenye jukumu la kushughulikia tatizo hili hatari mno kwa usalama wa taifa letu ni Idara ya Usalama wa Taifa.
Hata hivyo lengo la makala hii sio kujadili tena alichoongea Jenerali Mkunda bali kubainisha taarifa kuhusu mbunge mmoja ambaye ni jasusi wa nchi moja jirani anafanya jitihada za “jiweka karibu na Mama Samia.”
Na kana kwamba hilo sio baya vya kutosha, ukweli mchungu ni kwamba Idara ya Usalama wa Taifa inafahamu kuhusu suala hilo.