Milipuko ya Mabomu Uganda, Tahadhari ya Ugaidi Kenya, Mashambulizi ya Kigaidi Msumbiji, DRC ni "Wake-up Call" kwa Mzaha wa Kesi ya "Ugaidi" Dhidi ya Mbowe
Kuna jamaa yangu mmoja alinitumia ujumbe majuzi kunipongeza kuwa napaswa nijivunie jitihada zangu kwenye sekta ya intelijensia hususan kutupia jicho habari/matishio ya ugaidi.
Nilimshukuru lakini nilikataa pongezi hizo kwa sababu moja kuu. Hupaswi kujivunia kuwa mzalendo, kwa sababu uzalendo sio sifa bali wajibu. Kama ambavyo hatujivuni tunapokula, kwa s…