Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya (NIS) Noordin Haji afanya mabadiliko makubwa, amteua shushushu mzoefu Agnes Shikuku kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kwanza mwanamke
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya (NIS), Noordin Haji, (NIS), amefanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa juu wa taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kumteua naibu mkurugenzi mkuu mwanamke wa kwanza kabisa.