Mtandao: riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi - Sehemu ya Ishirini Na Tatu: "Giza Kabla Ya Mapambazuko"
Hii ni riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi. Matarajio ni kwamba riwaya hizi zitapelekea kuchapishwa kwa vitabu pindi zikimalizika.
Riwaya hii ya kwanza inaitwa Mtandao. Na makala hii inakuletea sehemu ya ishirini na moja.
Ili kupata mtiririko wa riwaya hii, unashauriwa usome sehemu 22 zilizopita ambazo links zake zipo kwenye makala hii
Aprili 8, 2023 – Saa Kumi Alfajiri
Mlio wa risasi ulitawala anga la Dar es Salaam. Giza la usiku lilianza kutoweka, likiwapa wapiganaji kivuli kidogo cha giza la alfajiri. Yvonne alikuwa tayari amepata njia ya kutuma nyaraka kupitia njia salama kwa mtu wa kuaminika serikalini. Joseph, akitetemeka kwa hofu, alikuwa chini, akiweka mikono kichwani, akijua kuwa usiku huu ungeweza kuwa wa mwisho kwake.