Mtandao: riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi - Sehemu ya Kumi Na Tisa: "AABD KiMMRUZ "
Hii ni riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi. Matarajio ni kwamba riwaya hizi zitapelekea kuchapishwa kwa vitabu pindi zikimalizika.
Riwaya hii ya kwanza inaitwa Mtandao. Na makala hii inakuletea sehemu ya kumi na tisa.
Ili kupata mtiririko wa riwaya hii, unashauriwa usome sehemu 18 zilizopita ambazo links zake zipo kwenye makala hii
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanznia, vitabu vinapatikana HAPA
Aprili 5, 2023
Baada ya mapumziko tangu awasili Arusha siku iliyopita, Jasusi aliamua kuwa kufanya mambo manne.
Kwanza, alifanya mawasiliano na Mama kumjulisha kuwa amefika. Mawasiliano kati yao sio tu yalikuwa kwa namba ya siri bali pia app aliyoitumia Jasusi kumpigia Mama isingeweza kudukuliwa kwa namna yoyote ile.
Licha ya kumjulisha kuwa Mama kuwa amefika, Jasusi alitumia fursa hiyo pia kumpatia mkuu huyo wa nchi maelezo mafupi ya jinsi atakavyompatia taarifa endapo itahitajika kufanya hivyo.
“Mwanangu, hizo taarifa zisije kuniua kwa presha bure maana nimeshapitia misukosuko mingi. Lakini wewe ndio mtaalamu, utakapoona muhimu kunipa taarifa, basi hakuna tatizo,” alisema Mama.