Mtandao: riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi - Sehemu ya Kumi Na Nane: "April wa Arachuga "
Hii ni riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi. Matarajio ni kwamba riwaya hizi zitapelekea kuchapishwa kwa vitabu pindi zikimalizika.
Riwaya hii ya kwanza inaitwa Mtandao. Na makala hii inakuletea sehemu ya kumi na nane.
Ili kupata mtiririko wa riwaya hii, unashauriwa usome sehemu 17 zilizopita ambazo links zake zipo kwenye makala hii
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana HAPA
April 3, 2023
Safari ya Jasusi kutoka Dubai hadi Addis Ababa iligharimu masaa manne unusu. Alikaa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa takriban masaa mawili kabla ya kupanda ndege ya kutoka hapo Ethiopia kuelekea Johannesburg, Afrika Kusini, safari iliyochukua masaa matano unusu hivi.
Alipofika Johannesburg alijisikia uchovu wa safari lakini alijimbia kimoyomoyo kuwa zege halilali, na kuamua kwamba asingelala hapo Afrika Kusini. Akachukua ndege nyingine hadi Nairobi, Kenya, safari iliyomgarimu masaa manne hivi.
Aliwasiliana na Yvonne aliyemshauri alale hapo Nairobi kwa usiku mmoja kisha kesho yake aelekee Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Lakini bila kufahamu, kumbe Yvonne alikuwa amemwandalia surprise [kitu cha kushtukiza]. Japo alishafahamishwa na Yvonne kuwa atamtuma mtu wa kumpokea, hakumwambia wasifu wa mtu huyo, na Jasusi hakuona haja ya kumdadisi jasusi mwezie wa Kikenya kwa sababu maamuzi yake siku zote ni sahihi.