Mtandao: riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi - Sehemu ya Ishirini Na Mbili: "Risasi Zarindima Dar"
Hii ni riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi. Matarajio ni kwamba riwaya hizi zitapelekea kuchapishwa kwa vitabu pindi zikimalizika.
Riwaya hii ya kwanza inaitwa Mtandao. Na makala hii inakuletea sehemu ya ishirini na moja.
Ili kupata mtiririko wa riwaya hii, unashauriwa usome sehemu 21 zilizopita ambazo links zake zipo kwenye makala hii
Aprili 7, 2023 – Usiku wa Manane
Dar es Salaam ilikuwa imeamka tayari na kero zake za usiku. Jiji hilo liliotawaliwa na mchanganyiko wa sauti za magari, muziki wa baa za uswahilini, na gumzo la wapita njia, lilionekana zuri na la kutisha kwa wakati mmoja. Gari la Jasusi lilikuwa limepaki kwa tahadhari kwenye kona ya giza karibu na Hoteli ya Serengeti Heights, ambapo mkutano wake wa kwanza ungefanyika.