Mtandao: riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi - Sehemu ya Ishirini: "Mwili Uliokatwa Kichwa 😯"
Hii ni riwaya (fiction) ya kwanza kabisa ya Jasusi. Matarajio ni kwamba riwaya hizi zitapelekea kuchapishwa kwa vitabu pindi zikimalizika.
Riwaya hii ya kwanza inaitwa Mtandao. Na makala hii inakuletea sehemu ya ishirini.
Ili kupata mtiririko wa riwaya hii, unashauriwa usome sehemu 19 zilizopita ambazo links zake zipo kwenye makala hii
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana HAPA
Arusha, Aprili 6, 2023
Moja ya ishara za kuiva kijasusi ni kuota ndoto zenye kuashiria mambo yajayo. Na usiku wa kuamkia siki hii, Jasusi aliota amekaa ufukweni akipunga upepo, lakini ghafla ikatokea treni inayotembea baharini lakini kichwa chake kimekatwa nusu na kinavuja damu. Treni hiyo ikawa inakuja kwa kasi kuelekea alipo Jasusi, na ikamlazimu kukimbia.
Aliposhtuka usingizini, Jasusi alijaribu kutafuta tafsiri ya ndoto hiyo. Kikubwa katika ndoto hiyo kilikuwa kichwa kinachovuja damu. Na kwa uzoefu wake, damu ilimaanisha kifo.
Lakini kama ni kifo kitakuwa cha nani? Au kundi la Mtandao lilikuwa limefahamu kuhusu ujio wa Jasusi na lilipanga kumuua? Au kundi lilipanga kumuua Mama? Au April?