Rai kwako Ndg Maulid Kitenge (@mshambuliaji) na wenzako mnaotetea mkataba wa bandari: msiturudishe zama za Musiba, teteeni bila kutudhihaki tunaoukosoa, hata sie mnaotukejeli "tulikimbia nchi"
Jana mdau mmoja alimfahamisha Jasusi kuwa watangazaji wa kituo kimoja cha habari huko nyumbani ambao wamejitanabaisha kuwa watetezi wa mkataba wa bandari kati ya Tanzania na Dubai, walimdhihaki Jasusi kama inavyoonyesha kwenye twiti hiyo hapo pichani.