Ripoti ya CAG: Maridhiano yamewafunga mdomo wapinzani kuongelea ufisadi uliobainishwa na CAG?
Hapana. Huu si mtazamo wa Jasusi. Hata hivyo, wadau mbalimbali, hususan wasomaji wa kijarida hiki, wameonyesha kuguswa na “ukimya” wa viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani kuhusu ufisadi wa kutisha uliobainishwa kwenye ripoti ya CAG iliyokabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu hivi karibuni.
Pengine wapinzani wanasubiri ripoti hiyo iwasilishwe rasmi bungeni …