Ripoti ya kiintelijensia: Habari adimu za kutia matumaini kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na jinsi DGIS Balozi Siwa anavyomudu "kulipa deni la matumaini kwake" (expectation debt)
Kwamba Idara ya Usalama wa Taifa imekuwa ikilaumiwa kwa mengi yanayojiri nchini Tanzania sio suala la siri hata kama taasisi hiyo inafanya kazi zake kwa usiri.
Kwamba Watanzania wengi wamepoteza matumiani kuiona taasisi hiyo nyeti na muhimu kabisa ikirudi zama za huko nyuma ambako ilisifika kwa umahiri wake barani Afrika, ambapo kwa upande mmoja iliweza kumudu kila hujuma zilizojaribiwa na utawala wa Makaburu wa Afrika Kusini, na kwa upande mwingine iliweza kufanikisha mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika.
Mafanikio haya hayafahamiki hata kidogo kwa sababu hayajawahi kuwekwa katika maandishi, changamoto ikiwa taasisi hiyo kuendelea kukumbatia usiri kupindukia hata katika maeneo yasiyohitaji usiri.
Hata hivyo, kuna habari njema kutoka kwenye taasisi hiyo.