Rwanda: huku kukiwa na tetesi za mapinduzi, Rais Kagame awatimua jeshini zaidi ya wanajeshi 200 ikiwa ni pamoja na mkuu wa zamani wa ushushushu nchini humo

Rais Paul Kagame amewatimua zaidi ya wanajeshi 200 kutoka jeshi la nchi hiyo, miongoni mwao wakiwa maafisa 14.
Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Rais Kagame kufanya mabadiliko makubwa katika taasisi za usalama na ulinzi nchini humo.