Safu ya BURUDANI na MICHEZO: Kombe la Mataifa ya Afrika - ubashiri wa akili mnemba kubaini atakayeibuka bingwa wa michuano hiyo
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 (Afcon) inaanza Jumamosi kwa wenyeji Ivory Coast kumenyana na Guinea-Bissau.
Kiu ya mamilioni ya washabiki wa soka barani Afrika na hata nje ya bara hilo sio tu katika kupata burudani ya soka na ushindi kwa timu wanazoshabikia bali pia kufahamu kuhusu nchi gani itaibuka kidedea.
Kwa Tanzania, kwa muda mrefu ubashiri kuhusu timu gani itashinda mechi ilikuwa shughuli ya wanajimu, maarufu zaidi akiwa marehemu Sheikh Yahya.
Lakini huu ni mwaka 2024, ambapo dunia ipo kwenye mwendo wa akili mnemba (artificial intelligence). Na akili mnemba imebashiri bingwa wa michuano hiyo muhimu.
Senegal ya Sadio Mane itaingia kwenye dimba hilo - lililotangazwa rasmi kama fainali za 2023 ingawa zinachezwa 2024 - kama mabingwa watetezi. Je, wana nafasi gani ya kushinda tena?