Safu ya MAISHA [Episode 4]: Mfahamu Zuhura Yunus (@VenusNyota), kutoka ndoto za kuwa daktari hadi utangazaji BBC Swahili, na sasa Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo
Moja ya majina mahiri kabisa katika tasnia ya utangazaji wa habari, hususan za Kiswahili, kimataifa ni Zuhura Yunus, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Tanzania. Aliteuliwa kushika wadhifa huo Februari 1, 2022 akiwa mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kushika wadhifa huo.