Samahani endapo makala hii itamkwaza mtu yeyote lakini ukweli shurti usemwe: kila atendaye maovu akumbuke pia kuwa kila nafsi itaonja mauti
Kwa mujibu wa mila na desturi zetu, “marehemu hasemwi vibaya.” Haifahamiki vizuri asili ya mila/desturi hiyo, lakini imekuwa kinga maarufu dhidi ya matendo mabaya yaliyofanywa na wenzetu kabla hawajatangulia mbele za haki.
Pengine sababu ya kukataza “kumsema vibaya marehemu” ni kuchelea kuwakwaza wafiwa. Lakini pia pengine ni kuzingatia ukweli kwamba “marehemu hawezi kujitetea” endapo anasingiziwa tu kuhusu ubaya anaodaiwa kuufanya wakati wa uhai wake.
Makala hii inaongelea misiba miwili mikubwa iliyojiri wiki iliyopita, ule wa majuzi wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, marehemu Bernard Membe, na huu wa jana wa bloga maarufu, marehemu William Malecela.