Sehemu ya Kwanza ya Mfululizo wa Makala Kuhusu Mmomonyoko wa Uzalendo Tanzania (Nilituma kwa Gazeti la Raia Mwema Lakini Haikuchapishwa)
MAKALA YA RAIA MWEMA
Evarist Chahali
Nianze makala hii kwa kuwataka radhi wasomaji kutokana na kuadimika kidogo. Hali hiyo ilisababishwa na sababu zilizo nje ya uwezo wangu.
Moja ya changamoto za uandishi wa makala kwenye gazeti kubwa kama hili la Raia Mwema ni ukweli kwamba matarajio ya wasomaji yapo juu sana. Kwa mantiki hiyo, mimi kama mwana-makala (col…