Siasa "zilivyopora" uchaguzi wa TLS ni kiashiria cha jinsi taaluma ya uanasheria inavyofeli katika utumishi kwa Watanzania hususan "wasio na vyama."
Moja ya taaluma ambazo Jasusi alikuwa anaziheshimu sana kwa Tanzania ni uanasheria. Na heshima hiyo ilianzia chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako Jasusi alisomea shahada yake ya kwanza.
Pale UDSM, wanafunzi wa sheria walikuwa na “mwonekano” tofauti na sie wanafunzi wengine. Kimsingi hata jengo la kitivo chao lilikuwa na mwonekano tofauti.
Wakati chuoni pa…