Soma tafsiri ya Kiswahili ya muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa 2023, na uchambuzi wa "mazuri" na "mabaya" yake
Jasusi amefanya tafsiri ya muswada wa Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya mwaka 2023 na kufanya uchambuzi wa “mazuri” na “mabaya” ya muswada huo.
Baada ya kusoma tafsiri hii, itakuwa rahisi kufahamu kwanini, kama alivyolalamika Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mheshimiwa Zitto Kabwe, mjadala kuhusu muswada huo huko Bungeni unafanyika kwa siri.
Kwa mnaofahamu kimombo, mnaweza kupakuwa muswada huo kwa lugha ya Kiingereza hapa chini
Hata hivyo, ikikupendeza, soma tafsiri ya Kiswahili rahisi kueleweka pamoja na uchambuzi wa kina kuhusiana na muswada huo, hususan jinsi ambavyo ukipitishwa - na hakuna uwezekano wowote usipitishwe - na kuwa sheria, itakuwa kikwazo kwa Katiba Mpya inayopiganiwa kwa nguvu kubwa muda huu.
Ifuatayo ni tafsiri ya Kiswahili rahisi kabisa kueleweka ya muswada huo, ikifuatiwa na uchambuzi wa “mazuri” na “mabaya” ya muswada/sheria tarajiwa