Taarifa za Ujio wa Mama @SuluhuSamia Hapa Uingereza: Makada wa CCM Waanza Kushawishi Watu "Kuunga Mkono Jitihada,"Jasusi "Awachomolea."
Kuna taarifa kuwa Mama Samia Suluhu atazuru hapa Uingereza hivi karibuni. Yawezekana ziara hiyo ikahusisha kuhudhuria mkutano wa mazingira unaofahamika kama COP26 unaofanyika katika mji huu ninaoishi wa Glasgow, hapa Uskochi.
Lakini kama ilivyo kawaida ya wana-CCM huko nyumbani na hata huku Ughaibuni, ziara za kitaifa za viongozi wakuu hutekwa na kugeuzw…