Tafakuri ya Kiintelijensia: Fursa na Vikwazo Kwa Uwezekano wa Chadema Kusalimika Baada ya Kumalizika kwa Uchaguzi Wake
Chadema itakamilisha mchakato wa uchaguzi katika ngazi mbali za uongozi wa chama hicho kwa, pamoja na nafasi nyingine, kumchagua Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho kikuu cha upinzani (kwa idadi ya wanachama).
Na ni nafasi hiyo ya Mwenyekiti ambayo sio tu imekuwa na ushindani mkubwa bali pia inaashiria kukipasua chama hicho kiasi cha baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa kuhisi kuwa huenda huu ukawa mwanzo wa mwisho wa chama hicho.
TANGAZO
Ikikupendeza, unaweza ku-preview nyimbo zote 15 zilizomo kwa albamu ya Jasusi ya #JasusiTheAlbum hapa
Katika tafakuri hii ya kiinteliensia, Jasusi anaangalia fursa na vikwazo kwa Chadema kusalimika baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Tafakuri hii ni ya kitaaluma (kiintelijensia) kwa asilimia 100, na hisia za Jasusi kuwa nani anafaa/hafai haziapewa fursa yoyote.