Tathimini fupi ya kiintelijensia kuhusu tuhuma dhidi ya JK, Kinana, GSM "kuhujumu mkataba wa bandari" - CCM waanza "kushikana uchawi" au ni mbinu tu ya kuhamisha mjadala?
Jana katika akaunti ya mmoja wa “waunga mkono” wa mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari, kulikuwa na tuhuma nzito dhidi ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana, na kampuni za GSM na Home Shopping Centre.
Mtoa tuhuma alidai kuwa watu hao wapo nyuma ya upinzani dhidi ya mkataba huo, akiwatuhumu kuwa ni wanufaika wa ukwepaji kodi kwa mfumo wa bandari uliopo kabla ya ujio wa kampuni ya DP World.
Makala hii infanya tathmini fupi ya kiintelijensia kuhusu tuhuma hizo kabla ya kuhitimisha endapo zina ukweli au la, na iwe zina ukweli au la, lengo ni nini hasa?