Tathmini fupi ya kiintelijensia kuhusu kukamatwa kwa Tundu Lissu jana na mustakabali wa maridhiano kati CCM na Chadema na siasa za Tanzania kwa ujumla
Kilichojiri: jana, Makamu Mwenyekiti wa Chadema na mgombea urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi mkuu wa 2020, Tundu Lissu alikamatwa na Jeshi la Polisi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Lissu alikamatwa jana Karatu Arusha, alikokuwa anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mazingira Bora.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, Lissu, mbunge wa zamani na mwanasheria, ambaye aliwahi kunusurika kuuawa kwa kupigwa risasi 16 miaka 6 iliyopita anatuhumiwa kwa makosa mawili; kufanya mikusanyiko bila kuwa na vibali na kuzuia Polisi kufanya kazi yao.
Kwa mujibu wa viongozi wa CHADEMA, kabla ya kumamatwa kwa Lissu, hoteli aliyofikiwa kiongozi huyo inayoitwa Ngorongoro na nyingine ya Panorama huko Karatu zilizingirwa na Polisi.
Hata hivyo baadaye Lissu na wenzake waliachiwa kwa dhamana kama anavyoeleza mwenyewe kwenye video hii hapa chini