Tathmini ya kiintelijensia: FURSA na CHANGAMOTO kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa Balozi Ali Siwa [Sehemu ya Kwanza: FURSA]
Juzi, Rais Samia Suluhu alimteua Balozi Ali Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa kufuatia kutumbuliwa kwa aliyekuwa anashika nafasi hiyo, Saidi Masoro.
Kufahamu sababu zilizopelekea Masoro kutumbuliwa, soma uchambuzi huu wa kiintelijensia
Kabla ya kuingia kwenye tathmini hii, Jasusi anapenda kuweka wazi ukweli kwamba yeye ni mwanafunzi wa Balozi Siwa, na tathmini kwa kiasi flani itaegemea kwenye ufahamu binafsi wa Jasusi kwa kiongozi huyo mpya wa taasisi hiyo nyeti. Hata, ufahamu huo hautoathiri tathmini hii kwani ipo “objective” na sio “subjective”.
Vilevile, kama ilivyokuwa kwa Jasusi, Mkurugenzi Mkuu aliyeondolewa, Masoro, naye alikuwa chini ya Balozi Siwa kimadaraka wakati mkuu huyo mpya alipokuwa Mkurugenzi wa Operesheni za Ndani (DOI).
Tathmini hii inaangalia FURSA (opportunities) na CHANGAMOTO (challenges) kwa Balozi Siwa katika wadhifa wake huo mpya.