Tathmini ya kiintelijensia: kuachiwa kwa Dkt Slaa na wenzake, na "kuyeyuka" kwa tuhuma za uhaini
Kabla ya kuingia kwenye tathmini hii, angalia video ya Jasusi kwenye makala hii iliyochapishwa jana ambayo inaweza kukupa mwangaza kuhusu kwanini Serikali ya Rais Samia Suluhu imeamua kuachana na tuhuma za uhaini dhidi ya Dkt Willibrord Slaa, Boniface Mwabukusi na Mdude Nyangali , na hatimaye kuwezesha jeshi la polisi kuwaachia huru watuhumiwa hao kwa dhamana.
Tathmini hii inatupia jicho sababu zilizopelekea kuyeyuka kwa tuhuma za uhaini na badala yake, Dkt Slaa na wenzake sasa wanatuhumiwa kwa uchochezi.
Taarifa za kiintelijensia zinaeleza kuwa tuhuma za uhaini dhidi ya Dokta Slaa, Mwabukusi na Mdude ni miongoni mwa yaliyojadiliwa katika kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika Alhamisi huko Dodoma