Tathmini ya kiintelijensia kuhusu fursa na changamoto kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa, Said Masoro [Sehemu ya Kwanza: Fursa]
Juzi, Januari 3, Rais Samia Suluhu alimteua Said Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Masoro aliteuliwa kushika nafasi hiyo nyeti kabisa kufuatia mtangulizi wake, Diwani Athumani, kuondolewa na kupewa nafasi ya Ukatibu Mkuu Ikulu.
Hata hivyo Diwani amekataa nafasi hiyo.
Masoro ni veterani wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Ameshika nyadhifa kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa mwambata ubalozini na nafasi yake kabla ya kupewa Ukurugenzi Mkuu alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu (Deputy Director General of Intelligence Service kwa kifupi DDGIS) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Operesheni za Ndani (Director of Internal Operations kwa kifupi DOI).
Makala hii ni sehemu ya kwanza ya tathmini ya kiintelijensia kuhusu fursa na changamoto kwa Masoro katika wadhifa wake huyo mpya wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, taasisi ambayo ndiyo roho ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika sehemu hii ya kwanza, zinaangaliwa fursa pekee. Sehemu ya pili itakayochapishwa kesho itahusu changamoto