Tathmini ya kiintelijensia: kuna tatizo mtoto wa Rais (Mama Samia) kukutana na Rais Museveni Ikulu Uganda?
Jana Rais Yoweri Museveni alitwiti kuhusu mkutano wake na Abdul Halim Hafidah Ameir.
Tafsiri
Nilikutana na Mheshimiwa Abdul Halim Hafidah Ameir na ujumbe wake kutoka Tanzania. Tulijadili ushirikiano wa siku za usoni katika eneo la Nishati, hasa njia ya umeme kutoka Mutukula hadi Mwanza, ambayo itaongeza usambazaji katika eneo hilo, na kusababisha maendeleo kwa Uganda na Tanzania.
Pia nilikubali pendekezo la wajumbe la kuendelea na kutengeneza mtambo wa kuzalisha umeme wa jua wa Megawati 20 katika wilaya ya Nwoya, karibu na kituo kidogo cha Olwiyo. Umeme huu utahamishwa kwenye gridi kuu na huko hatutakuwa tena na masuala ya umeme katika eneo hilo.
Kama huijui vema familia ya Rais Samia Suluhu basi utambue kuwa Abdul ni mwanae.
Baada ya twiti ya Rais Museveni na picha hizo akiwa na Abdula kusambaa, kukaibuka mjadala mzito huku baadhi ya watu wakihoji mtoto huyo ameenda Uganda kukutana na Rais Museveni kama nani.
Baadhi wakaenda mbali zaidi na “kuingiza habari za DP World” alimradi kuna mengi yaliyosemwa kuhusiana na tukio hilo.
Je ni tatizo kwa mtoto huyo wa Rais kukutana na Rais Museveni huko Uganda? Tathmini hii inatoa majibu yenye sura mbili. Moja ya “kiraia” na nyingine ya kiintelijensia.