Tathmini ya kijasusi: "yanayosemwa" kuhusu mabadiliko madogo ya kabineti ya Mama Samia yana ukweli au uzushi tu?
Kwa kifupi
Nini? Mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri la Rais Samia Suluhu.
Lini? Juzi Februari 14, 2023
Nani? Mohammed Mchengerwa, Pindi Chana, Hassan Abbas Said, Profesa Eliyamani Sedoyeka, Said Othman Yakub
Wapi? Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Kwanini? Hakuna maelezo rasmi yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu aliyeamua kufanya mabadiliko hayo, na kimsingi halazimiki kutolea maelezo kuhusu mabadiliko hayo au mengineyo.
Kivipi? Hapana inahusu taarifa hizo zimepokelewaje. Kwa Watanzania wengi, mabadiliko hayo ni kama mengine tu. Hata hivyo, kuna “vijimaneno” vimesambaa kuhusu baadhi ya wateuliwa, huko wawili kati yao wakitajwa kuwa ni “wakwe” wa Rais, na katika “vijimaneno” hivyo, inatafsiriwa kama mabadiliko hayo ni ya “kimaslahi binafsi” zaidi. Vilevile, kuna tuhuma za wanyamapori kutoroshwa kupelekwa Uarabuni, ambazo licha ya serikali kuzikanusha, zimeendelea kuvuma huku video kadhaa za “madege makubwa yanayotua mbugani” zikiwekwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa kirefu (na tathmini ya kiintelijensia)
Kuna masuala makuu sita yanayohusiana na mabadiliko hayo.
Waziri Pindi kutoka “wizara muhimu” kupelekwa “wizara sio muhimu sana”.
Kuhamishwa tena Waziri Mchengerwa, hii ikiwa ni wizara yake ya tatu katika mwaka mmoja na miezi 11 ya urais wa Rais Samia
Kuondolewa Profesa Madokeya
Katibu Mkuu Abbas kutoka “wizara si muhimu sana” kupelekwa “wizara muhimu” sambamba na uhusika wake kwenye Royal Tour.
Tuhuma za usafirishwaji wanyamapori
Kupanda kwa Katibu Mkuu Yakub