TEKLA, a love story: Riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi...japo hii si ya kijasusi ๐[Sehemu ya Kumi na Nane- "Njoo Nikuliwaze"]
Karibuni kwenye riwaya nyingine kutoka kwa Jasusi baada ya ile ya kwanza ya โMtandaoโ ambayo wengi wenu mmeipokea vizuri. Asanteni sana.
โTekla - a love storyโ ni stori ya kutunga kama ilivyo hiyo ya kijasusi ya โMtandao.โ Kwa vile lengo la Jasusi ni kukuletea simulizi ambazo ukisoma utajisikia kama unaangalia filamu, ni rahisi kudhani kuwa yanayoongelewa ni matukio ya kweli.
Kabla ya kuingia sehemu hii ya kumi na nane ya riwaya hii ya kimahaba, ni vema ukijikumbusha sehemu zilizopita ambazo kwa pamoja zipo katika makala hii
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana HAPA
Ilifanyika kazi ya ziada kumtoa James kaburini kwa sababu alitaka azikwe na mama yake. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Alitamani kufa kwa sababu haikumwingia akilini kama angeweza kuishi bila mama yake kuwa hai.
Kilichomfanya aweze kutoka kaburuni humo ni kilio cha Tekla ambaye alikuwa akilia kwa sauti akidhani kuwa James nae amefariki.
โMama katutoka, na wewe pia unanitoka Jamesโ, alisema Tekla huku analia.