Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu madai ya Chadema kumtaka Rais Samia awalete Scotland Yard kuchunguza utekaji; awatimue Masauni, IGP, DCI, DGIS; faida/hasara za kutekeleza/kutotekeleza madai hayo
Jana, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliongea na waandishi wa habari na kutoa chamko la chama chake kuhusu kifo cha kiongozi mwandamizi wa chama hicho, marehemu Ali Mohamed Kibao, sambamba na “kupotea” kwa makada mbalimbali wa chama hicho, na matukio ya utekaji kwa ujumla.
TANGAZO
Makala hii inahusu uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu aliyoongea Mheshimiwa Mbowe na tafsiri zake pana, sambamba na kukazia jicho hli inayofahamika kama “Catch-22” inayomkabili Rais Samia Suluhu, yaani kutekeleza au kutotekeleza matakwa ya Chadema kutamweka katika wakati mgumu.