Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu kung'olewa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Diwani Athumani, na kuteuliwa kwa Said Masoro kushika wadhifa huo nyeti
Jana Januari 3, 2023 Rais Samia Suluhu alimng’oa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani Msuya, na badala yake kumteua veterani wa Idara hiyo, Said Masoro, kushika wadhifa huo nyeti.
Ikumbukwe tu kuwa Jasusi sio tu alibashiri mara kadhaa huko nyuma kuwa Diwani angeng’olewa
Baada ya IGP Sirro, afuataye ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani. Ni suala la "lini" na si "endapo"
𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 @Chahali
lakini pia majuzi Jasusi alieleza jinsi Diwani anavyoikongoroa Idara hiyo na kuuweka mustakabali wa urais wa Rais Samia katika wakati mgumu.
Pamoja na mambo mengine, uchambuzi huu wa kiintelijensia unatanabaisha sababu za Diwani kung’olewa sambamba na kugusia kuhusu mrithi wa Diwani, yaani Masoro, na endapo kuteuliwa kwake kutaleta mabadiliko yoyote.