Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Mama Samia kumteua Makonda kuwa mwenezi CCM, ni wadhifa wa mpito tu, anaandaliwa "makubwa zaidi".
Jana Oktoba 22 ya mwaka huu 2023, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangaza kumrejesha kada wake Paul Makonda katika medani za uongozi baada ya kumteua kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unabainisha sababu halisi zilizopelekea uteuzi huo sambamba na kudokeza kuhusu “makubwa yajayo”.
Kwanini Mama Samia amemrudisha Makonda?
Kichwa cha habari kinasema “…Mama Samia kumteua Makonda kuwa mwenezi CCM…” japo barua ya uteuzi huo iliyotolewa na chama hicho inasema kuwa uteuzi huo umefanywa na Halmashauri Kuu ya CCM.